JE, WEWE NI WA ULIMWENGU HUU?
Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Warumi 12:2
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Tumezaliwa mara ya pili, tumekuwa kiumbe kipya, tumezaliwa na Mungu. Tuuvue mwenendo wa kwanza utu wa zamani unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya, na tufanywe upya katika roho ya nia zetu. Kwa hivyo, tusiwe wajinga, bali tufahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana. PAMOJA TUNAISHI KATIKA ULIMWENGU HUU, SISI SI WA ULIMWENGU HUU.
ambaye alijitoa nafsi yake [Yesu Kristo] kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu.
Wagalatia 1:4
mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.
Waefeso 4:24
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
2 Wakorintho 5:17
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mwanzo 1:26
Comments
Post a Comment