NI JINSI GANI TUNAPASWA KUTOA REHEMA?
mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.
Warumi 12:8
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tumepewa karama mbalimbali ikiwemo kurehemu kwa furaha. Pendo lisiwe la kinafiki, tuchukie maovu, tuambatane na yaliyo mema. Tubariki wanaotuudhi wala tusilaani. Tusilipe ovu kwa ovu.
Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.
Warumi 12:14
Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
2 Wakorintho 9:7
Comments
Post a Comment