NI NINI HATMA YA WALE AMBAO WATAONGEZA AU KUPUNGUZA MANENO YA UNABII?
Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.
Ufunuo wa Yohana 22:18-19
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Usisikilize viongozi wa uwongo ambao wanatafuta faida, usisikilize sauti zao zinazodanganya. Uliza kitabu ha mwongozo, Biblia kutoka Mbinguni; tumepewa kurasa zake kwa ajili ya wokovu wetu, ikiwa unatafuta njia ya kweli.
Msiliongeze neno niwaamurulo wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za Bwana, Mungu wenu, niwaamuruzo.
Kumbukumbu la Torati 4:2
Neno niwaagizalo lo lote liangalieni kulifanya; usiliongeze, wala usilipunguze.
Kumbukumbu la Torati 12:32
Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.
Ufunuo wa Yohana 22:7
ULIZA KITABU CHA MWONGOZO, BIBLIA KUTOKA MBINGUNI.
Comments
Post a Comment