NI ROHO GANI INAPASWA KUONGOZANA NA SALA?
Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
Marko 11:25
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Ili Baba yetu wa mbinguni atusamehe inatubidi tuwasamehe watu wote waliotukosea kwanza, na ndipo tusimame na kusali. Roho yako inatakiwa iwe safi, isiwe na neno juu ya mtu yoyote usalipo.
Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.
Mathayo 5:23-24
[Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]
Marko 11:26
Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
Marko 11:24
Comments
Post a Comment