NI UHUSIANO GANI UNAOENDELEA KATI YA BABA NA MWANA?
Mimi na Baba tu umoja.
Yohana 10:30
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Huu ndio uhusiano uliopo kati ya Mungu na mwana wake mpendwa Kristo Yesu. Hakuna alilofanya Bwana wetu Yesu Kristo kwa mapenzi yake mwenyewe, ila aliyoambiwa na Baba aliyemtuma kwetu. Kusudi lao ni moja. Mwana hakushuka kutoka mbinguni ili ayafanye mapenzi yake, ila mapenzi yake Baba aliyemtuma.
Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.
Mimi nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli.
Yohana 5:30-31
Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.
Yohana 5:19
Comments
Post a Comment