TUTAOMBAJE MSAMAHA, NA NI MARA NGAPI TUSAMEHE?
Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
Mathayo 6:12
Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?
Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.
Mathayo 18:22
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Ukisamehe sahau kabisa, kama mashariki ilivyo mbali na magharibi. Usibaki na chochote moyoni mwako. Msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
Mathayo 6:14-15
Comments
Post a Comment