WAISRAELI WALIPATA WAPI CHAKULA NA KINYWAJI CHA ROHO WALIPOKUWA JANGWANI?
wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;
wote wakala chakula kile kile cha roho;
wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
1 Wakorintho 10:2-4
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Lakini pamoja na hayo wengi hawakumpendeza Mungu na waliangamizwa jangwani. Mambo haya yalikuwa mfano kwetu ili tusiwe wa kutamani mabaya kama wale walivyotamani. Yaliandikwa kwa jinsi ya mifano ili kutuonya sisi.
Tazama, nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu; nawe utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu wapate kunywa. Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli.
Kutoka 17:6
Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.
Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.
1 Wakorintho 10:20-21
Comments
Post a Comment