BADALA YA KUTAFUTA UONGOFU WA ULIMWENGU, NINI YATAKUWA MATUMAINI YA KANISA?
Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;
2 Timotheo 4:7
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Tutalitazamia tumaini lenye baraka na kuonekana kwa utukufu wa Mungu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo, kwa kumaliza mwendo tukiilinda imani, na tukiwa tumevipiga vita vilivyo vizuri.
Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
1 Wathesalonike 4:17
Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka.
1 Petro 5:4
Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu. Wafilipi 3:20, Warumi 5:2
Comments
Post a Comment