IKIWA KIFO SIO KUJA KWA KRISTO, JE ATAKUJAJE?
wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.
Matendo ya Mitume 1:11
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Baada ya Yesu kuwaambia watapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yao Roho Mtakatifu na watakuwa mashahidi wake katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, watu wawili wenye nguo nyeupe wakasimama karibu yao wakawaambia jinsi Yesu atakuja.
Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
Luka 21:27
Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.
Ufunuo wa Yohana 1:7
Comments
Post a Comment