JE, BWANA HATAPEWA WATU WA MATAIFA KUWA URITHI?
Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako.
Zaburi 2:8
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Alimuweka awe mfalme, na aihuburi amri, maana ndiye mwanawe aliyemzaa. Yesu Kristo alimtukuza Mungu hapa duniani, hali aliimaliza kazi ile aliyopewa aifanye.
Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
Danieli 7:14
Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.
Yohana 17:5
Comments
Post a Comment