JE, HALI YA MAISHA ITAKUWA MBAYA KABLA BWANA ATAKAPOKUJA?
lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.
2 Timotheo 3:13
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Ndivyo nyakati za mwisho ulimwengu hautakuwa na nafuu, hali itazidi kuwa mbaya kabla ya kuja Kristo. Wengine watajitenga na imani kwa kusikiliza roho zidanganyazo na mafudisho ya mashetani. Zitakuwa nyakati za hatari. Watayakataa mafundisho yeye uzima na kufuata nia zao wenyewe wakijipatia waalimu makundi makundi, watajiepusha wasisikie yaliyo kweli kwa kugeukia hadithi za uongo, kwa kuwa wana masikio ya utafiti.
Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?
Luka 18:8
Comments
Post a Comment