JE, INJILI INAPASWA KUHUBIRIWA KWA KIWANGO GANI KABLA YA ULE MWISHO?
Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
Mathayo 24:14
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Wengi watajikwaa, nao watasalitiana na kuchukiana, na makristo wa uongo na manabii wengi wa uongo watatokea wakidanganya wengi, wakitoa ishara kubwa na maajabu, wakiwapoteza hata wale wateule, na kuongezeka maasi yatakayosababisha upendo kupoa. Hapo pia injili (habari njema ya ufalme) ya kweli itahubiriwa katika ulimwengu wote na kuwa ushuhuda kwa mataifa yote.
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Mathayo 28:19-20
Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
Yohana 14:23
Comments
Post a Comment