JE, KATIKA MFANO WAKE WA NGANO NA MAGUGU, MWOKOZI YESU KRISTO ALISEMA NINI?
Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.
Mathayo 13:30
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Alifananisha Ufalme wa mbinguni na mtu aliyepanda mbegu njema ya ngano katika konde lake, na baadae watu walipolala akaja adui akapanda magugu katikati yake. Watumwa wa mwenye shamba huyo walitaka kwenda kukusanya magugu yale, ila aliwakataza wasikusanye wakazing'oa ngano pamoja nayo.
Akajibu, akasema, Azipandaye zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu;
lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu;
yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika.
Mathayo 13:37-39
Comments
Post a Comment