JE, KUTAKUWA NA AINA NGAPI ZA WATU DUNIANI WAKATI BWANA ATAKAPOKUJA?
Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
1 Wathesalonike 5:5
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Ndugu, kwa habari ya nyakati na majira mnajua siku ya Bwana yaja kama mwivi ajavyo usiku. Wasemapo kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo ghafula, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hawataokolewa. Basi wa mchana tuendelee kufarijiana na kujengana kila mtu na mwenzake, hivyo hivyo kama tunavyofanya. Zamani tulikuwa giza, bali sasa tumekuwa nuru katika Bwana, tuenende kama watoto wa nuru; kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli, tukihakiki ni nini impendezayo Bwana.
Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.
Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu.
1 Wathesalonike 5:7-8
Comments
Post a Comment