JE, MAMBO YALIYOFUNULIWA NI KWA AJILI YA NANI?
Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii.
Kumbukumbu la Torati 29:29
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Sheria ya Bwana ni kamilifu, huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa Bwana ni amini, humtia mjinga hekima. Mtu mkaidi ni chukizo kwake, bali siri yake ni pamoja na wanyofu. Tuwe waungwana tukilipokea neno kwa uelekevu, kwa kuyachunguza maandiko kila siku, kwa maana yamefunuliwa kwa familia ya wanadamu milele.
Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.
Amosi 3:7
Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia.
Yohana 5:39
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Matendo ya Mitume 1:8
Comments
Post a Comment