JE, NI NINI KISEMWACHO JUU YA TAFSIRI YA UNABII?
Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.
1 Wakorintho 2:13
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Tumshukuru Mungu siku zote kwa neema aliyotupa katika Kristo Yesu. Hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho wa Mungu ili tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.
Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
2 Petro 1:20
Comments
Post a Comment