JE, NI WANGAPI WATAPATA MALIPO WAKATI MWANA WA ADAMU ATAKUJA?
Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Mathayo 16:27
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kumfuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, amfuate. Mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yake, ataiona. Je, hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake? Fadhili ziko kwake Bwana, maana ndiye amlipaye kila mtu sawasawa na haki yake.
Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
Yohana 5:29
Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,
atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake;
Warumi 2:5-6
Comments
Post a Comment