JE, PETRO ALITHIBITISHA VIPI MAHUBIRI YAKE YA ZAMANI KUHUSU KUJA KWAKE KRISTO?
Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake.
2 Petro 1:16
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Yesu Kristo alipata heshima na utukufu kutoka kwa Mungu Baba, kwa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, "HUYU NI MWANANGU, MPENDWA WANGU, NINAYEPENDEZWA NAYE". Sauti hiyo waliisikia ikitoka mbinguni walipokuwa naye (Yesu Kristo) katika mlima ule mtakatifu. Msikilizeni yeye.
Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.
Mathayo 17:5
Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
2 Petro 1:19
Comments
Post a Comment