JE, WALE AMBAO WAPO GIZANI WATASEMA NINI WANAPOSIKIA JUU YA KUJA KWA BWANA?
Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,
na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.
2 Petro 3:3-4
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Ndugu, tuyakumbuke maneno hayo yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba, wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakifuata tamaa zao wenyewe za upotevu, waletao matengano, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho, wenye tabia ya asili wasiopokea mambo ya Roho wa Mungu.
Wasema, Na afanye haraka, aihimize kazi yake, tupate kuiona; na likaribie shauri lake aliye Mtakatifu wa Israeli, tupate kuliona.
Isaya 5:19
Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia;
bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua,
Mathayo 24:48,50
Comments
Post a Comment