JINSI MITI INAVYOCHIPUA NA KUCHANUA MAJANI, TUJIFUNZE NINI?
Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu;
Mathayo 24:32
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Wakati miti inachipuka na kuchanua majani yake, unatambua kuwa wakati wa mavuno u karibu. Vivyo hivyo tuonapo dalili zote alizotufundisha Kristo Yesu, tutambue kuwa yu mlangoni. Na akatuambi kizazi hiki hakitapita, hata yote yatakapotimia, akimaanisha kizazi kitakachoona dalili hizo za ule mwisho.
nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.
Mathayo 24:33
Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
Luka 17:34
Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Mathayo 24:35
Comments
Post a Comment