KATIKA KUTOA UTABIRI WA KINABII, MANABII WALITAFUTA NINI?
Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi.
1 Petro 1:10
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Katika kupokea wokovu wa roho zetu, twampenda Yesu Kristo ijapokuwa hatukumwona na hatumwoni hata sasa, twamwamini na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka yenye utukufu.
Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.
1 Petro 1:11
Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie.
Mathayo 13:17
Comments
Post a Comment