MANABII WA UONGO, MSIJALI, ENDELEENI NA HUO UONGO WENU.
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Ninyi manabii wa uongo, msiache, endeleeni, maana hamtakamatwa, tena msisahau Wakristo ni wepesi wa kusahau hayo mnayoyasema. Tena maandiko yanawaonya wasitweze unabii. Hivyo nyie endeleeni, hawataudharau unabii. Ila mkumbuke wanaopokea huo unabii (watu wa Mungu na watoto wa Mungu) wameambiwa kwenye maandiko, wafurahi sikuzote, wakiomba bila kukoma na wakishukuru kwa kila jambo, maana hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwetu katika Kristo. Na pia wasimzimishe Roho, wakijaribu mambo yote kwa kuyashika yaliyo mema, pamoja na kujitenga na ubaya wa kila namna. Watu wa Mungu hawaangamii, bali wanangamizwa kwa kukosa maarifa, kwa kuwa wewe kuhani umeyakataa maarifa. Lakini watoto wa Mungu wanayatafuta na wanayo maarifa, watawashtukia tuu uongo wenu, maana mnafahamika mpo kila mahali.
Hosea 4:6 na 1 Wathesalonike 5:16-23
Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
1 Yohana 4:1
Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
Mathayo 7:15
Comments
Post a Comment