NI AHADI GANI MAALUM, AMBAYO MWOKOZI ALITOA KUHUSU KUJA KWAKE TENA?
Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
Yohana 14:2-3
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Yesu ndiye njia, na kweli, na uzima, mtu haendi kwa Baba ila kwa njia ya yeye. Amwaminie yeye na kazi alizozifanya, huyo atazifanya, na kubwa kuliko hizo atafanya. Tumwamini Mungu, na tumuamini yeye (Kristo Yesu), tusifadhaike mioyoni mwetu.
Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
Yohana 14:13,23
Comments
Post a Comment