JE, AFANYAYE DHAMBI NI MTUMWA WA NANI?
atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.
1 Yohana 3:8
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Atendaye dhambi afanya uasi, maana dhambi ni uasi. Yesu alidhihirishwa ili aziondoe dhambi na kuzivunja kazi za ibilisi, na dhambi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi. Ibilisi alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe, sababu yeye pia ni muongo na baba wa huo, na hamna hiyo kweli ndani yake.
Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi.
1 Yohana 5:18
Comments
Post a Comment