JE, KUNA WATOA SHERIA WANGAPI?
Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine?
Yakobo 4:12
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi. Basi tusihukumu maana mtoa sheria na mwenye hukumu ni mmoja. Ndugu tusisingiziane au kuhukumuiana ndugu. Pia hatujui yatakayokuwa kesho, maana yeye anaweza kuokoa na kuangamiza.
Kwa hiyo, wewe mtu uwaye yote uhukumuye, huna udhuru; kwa maana katika hayo umhukumuyo mwingine wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia; kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale.
Warumi 2:1
Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha.
Warumi 14:4
Comments
Post a Comment