JE, MATUKIO NA SIRI ZA MUNGU NI NANI WANAFUNULIWA?
Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.
Amosi 3:7
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Bwana Mungu amenena, ni nani awezaye neno ila kutabiri? Hata Kristo Yesu aliwaita wanafunzi wake rafiki na sio watumwa sababu yote aliyoyasikia kwa Baba yake aliwaarifu. Midomo ya kuhani ihifadhi maarifa, maana ni mjumbe wa Bwana wa majeshi.
Maana mtu mkaidi ni chukizo kwa Bwana, Bali siri yake ni pamoja na wanyofu.
Mithali 3:32
Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili!
1 Wakorintho 9:16
Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana;
Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.
Ufunuo wa Yohana 1:1,19
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
2 Petro 1:21
Comments
Post a Comment