JE, MUNGU AMEWEKA SIKU YA HUKUMU?
Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.
Matendo ya Mitume 17:31
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Mungu anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu, maana sisi sote tuu wazao wake. Tumtafute Mungu, ingawa kwa kupapasa-papasa, tukamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu. Akaagiza watu wahubiriwe na kushuhudiwa ya kuwa Kristo Yesu ndiye aliyemuamuru awe Mhukumu wa walio hai na wafu, na kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi. Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki.
Mbele za Bwana, kwa maana anakuja, Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa uaminifu wake.
Zaburi 96:13
Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa.
1 Petro 4:5
Comments
Post a Comment