JE, MUNGU ANAMWANGALIA MTU WA NAMNA GANI?
Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.
Isaya 66:2
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Mbingu ni kiti chake cha enzi, na nchi(dunia) ni pa kuwekea miguu yake. Je, ni nyumba gani mtakayomjengea, au ni mahali gani atakapostarehe, si kwa mkono wake uliofanya haya yote? asema Bwana. Hakai katika nyumba zilizofanywa kwa mikono. Bwana yu katika hekalu lake takatifu, ambapo kiti chake kiko mbinguni.
Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa.
Zaburi 34:18
Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.
Zaburi 51:17
Comments
Post a Comment