JE, MWOKOZI ALISEMA NINI KUHUSU KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU?
Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
Mathayo 7:21
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Alisema tuihadhari na manabii wa uongo, watu wanaotujia wamevaa mavazi ya kodoo, kumbe ni mbwa mwitu. Mtawatambua kwa matunda yao, maana mti mwema huzaa matunda mazuri, na mti mwovu hazaa matunda mabaya. Tuyafanye mapenzi ya Baba yetu wa mbinguni hapa duniani. Mtu anatakiwa kuwa na imani yenye matendo mema (mapenzi ya Mungu).
Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.
Yakobo 1:22
Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa?
Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.
Yakobo 2:14,26
Comments
Post a Comment