JE, MWOKOZI ATATOKEAJE KWA WALE AMBAO HATIMAYE WANARUHUSIWA KUMWONA?
Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.
1 Yohana 3:2
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Tukae ndani yake, ili kusudi atakapofunuliwa tuwe na ujasiri, wala tusiaibike mbele zake katika kuja kwake. Mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, hivyo kila atendaye haki amezaliwa na yeye. Kama tu watoto, tu warithi wa Mungu pamoja na Kristo, tukiteswa pamoja naye ili tupate kutukuzwa pamoja naye.
atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.
Wafilipi 3:21
Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu.
Wakolosai 3:4
Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.
1 Yohana 3:3
Comments
Post a Comment