JE, NI AHADI GANI ILIYOTOLEWA KWA WALE WANAOKIRI DHAMBI ZAO?
Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
1 Yohana 1:9
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Tukisema kwamba hatuna dhambi au kwamba hatukutenda dhambi twajidanganya wenyewe na kumfanya Mungu mwongo, wala kweli haimo mwetu na neno lake halimo mwetu. Yeye ni mwema sana na mwaminifu sana na wa haki.
Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
Mithali 28:13
Comments
Post a Comment