JE, NI NAMNA GANI TUNATAKASWA TUTOKE KATIKA DHAMBI?
bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.
1 Yohana 1:7
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Kwa damu yake Kristo Yesu ambaye kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itasafisha dhamiri zetu na matendo maovu tupate kumwabudu Mungu. Hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu, tumepata utakaso.
tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake,
Ufunuo wa Yohana 1:5
Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;
bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
1 Petro 1:18-19
Comments
Post a Comment