JE, TOBA YA KWELI INAHUSISHA NINI?
Tupilieni mbali nanyi makosa yenu yote mliyoyakosa; jifanyieni moyo mpya na roho mpya; mbona mnataka kufa, enyi nyumba ya Israeli?
Ezekieli 18:31
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Ukirudi, ukaghairi, na kuyaacha makosa yako yote, uovu wako hautakuwa uharibifu kwako. Msienende tena kama Mataifa waenendavyo, ambao akili zao zimetiwa giza, wamefarakanishwa na uzima wa Mungu, sababu ya ujinga ndani yao na ugumu wa mioyo yao. Mvue mwenendo wa kwanza utu wa zamani kwa kufuata tamaa zenye kudanganya na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu.
mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.
Waefeso 4:24
Comments
Post a Comment