JE, NI NINI PAULO AMBACHO ALISEMA ANAKISUBIRI?
baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.
2 Timotheo 4:8
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Baada ya kuona wakati wake wa kufariki umefika, alisema amevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo ameumaliza, na imani ameilinda. Anachosubiri ni siku ile ya kupewa taji ya haki aliyowekewa, na sio yeye tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake Bwana.
Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka.
1 Petro 5:4
Hata mtu akishindana katika machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali.
2 Timotheo 2:5
Comments
Post a Comment