KRISTO KWENYE KUBADILIKA AKIWAKILISHA UTUKUFU WAKE WA BAADAE, ALIONEKANAJE?
akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang'aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
Mathayo 17:2
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Petro, Yakobo na Yohana walipojulisha nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake, hawakufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, bali walikuwa wameona wenyewe ukuu wake. Alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu, walipokuwa pamoja naye katika mlima ule mtakatifu, waliposikia sauti ikitoka mbinguni katika utukufu mkuu "Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye".
Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.
Mathayo 17:5
Comments
Post a Comment