KWA NINI UTEKELEZAJI WA HUKUMU AMEPEWA KRISTO?
Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.
Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu.
Yohana 5:26-27
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Baba ampenda Mwana, naye humwonyesha yote ayatendayo mwenyewe, hata kubwa zaidi kuliko hizo atamwonyesha, ili tupate kustaajabu. Watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyempeleka.
Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.
Matendo ya Mitume 17:31
Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote;
Yohana 5:22
Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
Danieli 7:14
Comments
Post a Comment