MTUME ANAITAJE KANISA AMBALO LIMEHARIBIWA NA USHIRIKIANO WA KIDUNIA?
Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.
Yakobo 4:4
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Ameliita kuwa ni adui wa Mungu, hata laomba, wala halipati kwa sababu laomba vibaya ili livitumie kwa tamaa zake. Nia ya mwili ni mauti, na ni adui juu ya Mungu, hautii sheria za Mungu, wa hauwezi kutii. Kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia, na inapita, pamoja na tamaa zake.
Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
1 Yohana 2:15
Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
Warumi 8:8
Comments
Post a Comment