NEEMA YA MUNGU INATUFUNDISHA NINI?
Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
Tito 2:11-12
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Tusiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia; maana mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali tudumu katika kuyafanya mapenzi ya Mungu hata milele. Katika Kristo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.
kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.
Waefeso 1:4,6
Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
1 Yohana 2:16
Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.
Yakobo 4:17
Comments
Post a Comment