NI NANI ATAKAYEHUKUMIWA NA WATAKATIFU, NA NI WAKATI GANI?
Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo?
Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?
1 Wakorintho 6:2-3
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu.
Neema na amani zitokazo kwa Yesu Kristo, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia, ametupenda na kutuosha dhambi zetu katika damu yake; ametufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, kwa utukufu na ukuu alio nao milele na milele.
Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
Ufunuo wa Yohana 3:21
Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.
1 Wakorintho 4:5
Comments
Post a Comment