NI NINI TABIA YA MATENDO YA MUNGU?
Matendo ya mikono yake ni kweli na hukumu, Maagizo yake yote ni amini,
Yamethibitika milele na milele, Yamefanywa katika kweli na adili.
Zaburi 111:7-8
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Sheria ya Bwana kamilifu, huiburudisha nafsi. Ushuhuda wake ni amini, humtia mjinga hekima. Maagizo yake ni ya adili, huufurahisha moyo. Amri yake ni safi, huyatia macho nuru. Hukumu zake ni kweli, zina haki kabisa. Zinaonya; na kuzishika kuna thawabu nyingi.
Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.
Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.
Ufunuo wa Yohana 15:3-4
Comments
Post a Comment