NI NINI TABIA YA SHERIA YA MUNGU?
Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.
Warumi 7:14
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Torati si dhambi, na tusingalitambua dhambi ila kwa sheria; mfano tusingejua kutamani, kama torati isingalisema , Usitamani. Kuyajua mapenzi ya Mungu, na kuyakubali mambo yaliyo bora, umeelimishwa katika torati.
Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.
Zaburi 51:5
Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
Yohana 3:6-7
Comments
Post a Comment