WAAAMINI HAWA UTAISHI.
Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
Yohana 14:1
Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.
Luka 10:28
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. TUMUAMINI MUNGU, BABA YETU ALIYE MBINGUNI. TUMUAMINI YULE (KRISTO YESU) ALIYETUMWA NA YEYE (MUNGU). TUMUAMINI ROHO MTAKATIFU, AMBAYE KRISTO ALITUOMBEA KWA BABA ATUPE AWE MSAIDIZI WETU YEYE ALIPOONDOKA.
Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye.
Yohana 6:29
Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Yohana 14:16-17
Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
Yohana 14:12
Comments
Post a Comment