IKIWA KWELI AMEZALIWA NA MUNGU, MTU ATADHIHIRISHA VIPI?
Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.
1 Yohana 4:7
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Atadhihirisha kwa upendo alio nao kwa watu wote. Asiyependa hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo. Pendo la Mungu lilionekana kwetu kwa kumtuma Mwanawe pekee ulimwenguni ili tupate uzima wa milele. Si kwamba sisi tulimpenda Mungu, ila yeye alitupenda sisi. Ikiwa Mungu alitupenda sisi kwa kiasi hichi, inatupasa na sisi kupendana. Tukipendana Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu kwa kuwa ametushirikisha Roho wake.
Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.
Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.
1 Yohana 4:16,21
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Yohana 3:16
Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.
Warumi 5:8
Comments
Post a Comment