IKIWA MTU HAUFUATI MWILI, NI NAMNA GANI ANAKUWA SALAMA?
Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
Warumi 8:9
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Mtu anakuwa salama sababu Roho wa Mungu anakaa ndani yake. Nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, na wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu, na Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu, warithi w Mungu, turithio pamoja na Kristo, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
1 Wakorintho 3:16
Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu.
1 Wakorintho 12:3
Comments
Post a Comment