JE, HIZI MBILI, ROHO NA MWILI ZINAPATANA?
Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
Wagalatia 5:17
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Tukienenda kwa Roho, hatutazitimiza kamwe tamaa za mwili. Mkiongozwa na Roho, hampoa chini ya sheria. Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili mwataka kufa; bali mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.
Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
Wagalatia 6:8
Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
1 Petro 2:11
Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.
Warumi 8:14
Comments
Post a Comment