JE, KRISTO HUUNGANISHWA NA WANAFUNZI WAKE KWA MFANO GANI?
Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
Yohana 15:5
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Huunganishwa na wanafuzi wake kwa mfano wa mzabibu na matawi. Yeye ndani yetu na sisi ndani yake. Yeye ndiye ndiye mzabibu, sisi matawi na Baba yetu aliye Mbinguni ndiye mkulima. Kila tawi ndani yake lizaalo hulisafisha lizidi kuzaa, na tawi lisilozaa huliondoa. Wafuasi wake wamekwisha kuwa safi kwa sababu ya neno lake. Tawi haliwezi kuzaa peke yake lisipokaa ndani ya mzabibu, hivyo sisi tusipokaa ndani yake na yeye ndani yetu. Tukikaa ndani yake, na maneno yake yakikaa ndani yetu, lote tutakalo tukiomba tutatendewa.
Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
Yohana 15:8
Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake.
1 Wakorintho 12:27
Comments
Post a Comment