JE, KUZALIWA UPYA HUFANYA MAISHA YA AINA GANI?
Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.
Warumi 6:11
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Mtu anakuwa hai kwa Mungu katika Kristo Yesu. Fahamu kuwa tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake. Tulizikwa pamoja naye kwa huo ubatizo, kusudi kama alivyofufuka katika wafu kwa utukufu wa Baba, na sisi tuenende katika upya wa uzima. Tulivyounganika na Kristo katika mfano wa mauti yake, tutaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake.
tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.
2 Wakorintho 5:15
Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.
1 Petro 2:24
Comments
Post a Comment