JE, KWA NINI ULIMWENGU UNAMCHUKIA MKRISTO WA KWELI?
Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.
Yohana 15:19
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Twajua ulimwengu umemchukia Kristo kabla hata haujawachukia Wakristo wa kweli. Haya yote watatenda kwa ajili ya jina la Kristo kwa kuwa hawamjui Baba aliyempeleka. Yeye amchukiaye Kristo humchukia na Baba yake. Wa dunia hunena ya dunia na dunia huwasikia. Ulimwengu hauwezi kuwachukia Wakristo bila sababu; bali ni sababu ya Kristo kuushuhudia kazi zake ni mbovu. Ndugu zangu, msistaajabu, ulimwengu ukiwachukia.
Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
Yohana 17:14
Heri ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.
Luka 6:22
Comments
Post a Comment