JE, MATENDO YA ROHO (TUNDA LA ROHO) NI YAPI?
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
Mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria na walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Tutimize maagizo ya torati ndani yetu sisi tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho. Nia ya roho ni uzima na amani
kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli;
Waefeso 5:9
Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
Wagalatia 5:25
Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
1 Petro 2:11
Comments
Post a Comment