JE, MTU AKIKAA NDANI YA KRISTO, ANATAKIWA AENENDE NAMNA GANI?
Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.
1 Yohana 2:6
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Twajua tumo ndani yake kwa kulishika neno lake, na katika Kristo, upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Ukisema umemjua wala huzishiki amri zake ni mwongo, wala kweli haimo ndani yako. Kumpenda Mungu ni kwamba tuzishike amri zake wala si nzito. Tujitie nira ya Kristo, tujifunze kwake, kwa kuwa yeye ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nasi tutapata raha nafsini mwetu; kwa maana nira yake ni laini na mzigo wake ni mwepesi.
Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.
Yohana 15:10
Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.
Yohana 13:15
Comments
Post a Comment